Matokeo ya Darasa la Saba 2024 ikiwa na maana ya Primary School Leaving Examination (PSLE) yanayotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), ni hatua muhimu kwa wanafunzi na wazazi kote nchini Tanzania. Katika makala haya tutaonyesha zaidi jinsi ya kuangalia matokeo mikoa yote 2024/2025, mkoa wa Arusha, Dar es Salaam, Kagera, Mara, Mwanza, Pwani, Ruvuma, Tabora, Tanga, Katavi, Simiyu, Songwe, and Geita shule ya msingi pdf www.necta.go.tz standard seven 7 Results Here.
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania (NECTA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1973. NECTA ina jukumu la kusimamia mitihani yote ya Kitaifa na Tathmini nchini Tanzania.
Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE) ni hatua muhimu katika mfumo wa elimu nchini Tanzania, unaoathiri mustakabali wa wanafunzi wengi wanaohitimu elimu ya msingi. Katika mwaka wa masomo wa 2024/2025, matokeo ya mitihani hii yanatarajiwa kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwishoni mwa mwezi Novemba au mwanzoni mwa Desemba 2024. Matokeo haya siyo tu yanaashiria kiwango cha ufaulu wa wanafunzi, bali pia huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuwachagua wanafunzi watakaoendelea na elimu ya sekondari.
Mchakato wa Utoaji wa Matokeo ya Darasa la Saba
Katika Matokeo darasa la saba 2024, Mtihani unahusisha masomo manne, ambayo ni Hisabati, Sayansi, Kiswahili, na Kiingereza, ambapo kila somo linatathminiwa kwa alama 100. Mfumo wa utoaji alama unatumia madaraja A hadi F, ambapo daraja A ndilo bora zaidi. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, kiwango cha ufaulu mwaka huu kinatarajiwa kufikia 85.12%, ikiwa ni ongezeko kutoka mwaka uliopita
Baada ya kumalizika kwa mitihani, NECTA huchukua muda wa takribani miezi miwili hadi mitatu kuchakata na kuhakiki matokeo kabla ya kuyatangaza rasmi. Wanafunzi, wazazi, na walimu wanaweza kuyapata matokeo kupitia tovuti rasmi ya NECTA au kwa kutumia njia mbadala kama vile huduma za SMS.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2024/2025
Ili kuangalia matokeo ya darasa la Saba 2024/25, fuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kwa kubofya NECTA.
- Chagua sehemu ya Matokeo, kisha bonyeza kiungo cha “PSLE Results.” https://necta.go.tz/psle_results
- Chagua mkoa na wilaya yako, halafu chagua shule yako.
- Matokeo yatakuwa katika orodha, ambayo utaweza kupakua na kuangalia jina lako ili kuona alama zako.
Matokeo kwa SMS
Jinsi ya kuangalia kwa wale ambao hawana intaneti ya uhakika au kifaa cha kuvinjari, unaweza pia kuangalia matokeo kupitia huduma za SMS au USSD zinazotolewa na NECTA. Kuweza kufanya hivyo, Tuma ujumbe ukitumia namba yako ya mtahiniwa kwenda namba maalum iliyotolewa na NECTA, na matokeo yako yatatumwa ndani ya muda mfupi.
- Piga *152*00#
- Chagua namba 8. ELIMU
- Chagua namba 2. NECTA
- Chagua aina ya huduma 1. MATOKEO
- Chagua aina ya Mtihani 2. PSLE
- Andika namba ya Mtihani na Mwaka Mfano: PS0405007-0057
- Chagua aina ya Malipo (Gharama kwa kila SMS ni Tshs 100/=)
- Baada ya kukamilisha malipo utapokea ujumbe mfupi wa matokeo
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
IRINGA | KAGERA | KIGOMA |
KILIMANJARO | LINDI | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | PWANI | RUKWA |
RUVUMA | SHINYANGA | SINGIDA |
TABORA | TANGA | MANYARA |
GEITA | KATAVI | NJOMBE |
Zingatia: Matokeo yatakuwa katika mfumo ambao utaonyesha waliofanya mtihani, wastani wa ufaulu, madaraja ya ufaulu wa ujumla pia, ufaulu wa kila mwanafunzi. Ambapo katika jedwali litaonyesha
- Namba ya mtihani
- Jina la mwanafunzi
- Jinsia
- Masomo
Kwa wale ambao hawana uwezo wa kupata matokeo kwa njia ya mtandao, NECTA pia hutoa huduma ya kupata matokeo kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS). Njia hii ni ya haraka na rahisi kwa wanafunzi walio maeneo ambayo hayana mtandao imara wa intaneti.
Hatua za Baadae kwa Wanafunzi Waliofaulu
Baada ya matokeo ya la saba 2024 kutangazwa, hatua inayofuata ni mchakato wa baraza kutoa orodha ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari. Wanafunzi waliofaulu kwa alama za juu (A hadi C) watachaguliwa kujiunga na shule za sekondari za serikali, huku wale waliofanya vizuri zaidi wakiwa na nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na shule maarufu za kitaifa.
Kigezo muhimu cha kujiunga na kidato cha kwanza ni kufaulu kwa kiwango si chini ya daraja C. Wanafunzi wanaopata daraja A hadi C watakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa kujiunga na shule bora zaidi nchini
Umuhimu wa Matokeo ya PSLE
NECTA, Matokeo ya Mitihani ya darasa la saba 2024/2025 ni muhimu sana kwani hutoa msingi kwa wanafunzi kujiandaa na safari ndefu ya elimu ya sekondari na hatimaye elimu ya juu. Wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na shule za sekondari wanapaswa kujipanga kimasomo zaidi kwani kiwango cha ushindani huongezeka wanapoingia sekondari. Aidha, wazazi na walimu wana jukumu kubwa la kuwaongoza watoto wao katika kupanga malengo ya baadaye na kuwasaidia kuelewa umuhimu wa elimu.
Hitimisho:
Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba ya mwaka 2024/2025 ni tukio kubwa kwa wanafunzi na familia zao. Haya matokeo yanawasaidia wanafunzi kufahamu wapi wanapoelekea kielimu na pia hujenga msingi wa safari yao ya sekondari. Matokeo haya, yanayopatikana kupitia tovuti rasmi ya NECTA, ni hatua moja muhimu kuelekea mafanikio ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Tanzania.
SOMA ZAIDI: