Makala

Majina ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024

Majina ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024

Majina ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024 ( Usaili wa Walimu) yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu na walimu wengi wanaotafuta nafasi za ajira serikalini , Kwenye Makala Hii Tumekuandalia PDF ya walioitwa kwenye usaili kada ya ualimu 2024, Walimu walioitwa kwenye usaili serikalini Sekretarieti ya Ajira ajira.go.tz

Angalia hapa Matokeo

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs (Ministry, Departments, and Agencies) na LGAs (Local Government Authorities), amewataarifu Waombaji Kazi wa kada ya Ualimu kuwa usaili wa ajira unatarajiwa kuanza kuendeshwa kuanzia tarehe 02 Novemba 2024 hadi 15 Novemba 2024. Usaili huu ni kwa ajili ya kuwapangia vituo vya kazi wale wote watakaofaulu hatua hii ya usaili.

Waombaji walioshinda hatua za awali na walioitwa kwenye usaili wanashauriwa kujiandaa kikamilifu kwa tarehe zilizotajwa. Majina ya walioitwa kwenye usaili ajira za walimu 2024 yamechapishwa na yanapatikana katika tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira au kupitia tangazo rasmi.

PDF ya Majina ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024

Majina ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024

Ili kuangalia majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili wa kada ya ualimu, hatua zifuatazo zinaweza kukusaidia:

  1. Tembelea Tovuti Rasmi ya Sekretarieti ya Ajira: Nenda kwenye tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa kufuata kiunganishi: Sekretarieti ya Ajira
  2. Tafuta Sehemu ya Matangazo ya Kazi na Usaili:Baada ya kufika kwenye tovuti, nenda kwenye sehemu iliyoandikwa “Matangazo ya Kazi na Usaili” au “Tangazo la Walioitwa Kwenye Usaili”. Hii inapatikana katika ukurasa wa mwanzo au sehemu ya matangazo.
  3. Bonyeza Kiungo cha Walioitwa Usaili Kada ya Ualimu:Ukishaingia kwenye sehemu ya matangazo, utaona orodha ya tangazo lenye kichwa cha habari kinachosema “Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu 2024”. Bonyeza kiungo hicho ili kufungua ukurasa wa tangazo.
  4. Pakua Faili ya PDF: Baada ya kubonyeza tangazo, utapata kiungo cha kupakua PDF ya Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Kada ya Ualimu. Bonyeza kitufe cha kupakua ili kuipata PDF hiyo kwenye kifaa chako.
  5. Angalia Majina Yako: Fungua PDF iliyopakuliwa na tumia kipengele cha kutafuta (search) ili uangalie jina lako kwenye orodha kwa urahisi. Hakikisha unafuata maelekezo ya tarehe, muda, na mahali pa kufanyia usaili.

SOMA ZAIDI: NECTA Matokeo ya Darasa la Saba 2024/2025 PSLE

Maelezo Muhimu Kuhusu Usaili

Tarehe za Usaili: Kuanzia tarehe 02 Novemba 2024 hadi 15 Novemba 2024. Mahali: Usaili utafanyika katika maeneo yaliyotengwa na Sekretarieti ya Ajira. Waombaji wanatakiwa kufuatilia mahali husika kama ilivyoelekezwa kwenye tangazo.

Nyaraka Muhimu: Hakikisha unakuwa na nyaraka zako zote muhimu ikiwemo barua ya kuitwa kwenye usaili, vyeti vya elimu, kitambulisho cha taifa, na vielelezo vingine vinavyohitajika.

Kwa waombaji wa kada ya afya pia, mchakato wa kuangalia majina yao unafanana na huu. Tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira na fuata hatua hizi kuangalia majina ya walioitwa kwenye usaili wa kada ya afya.

DOWNLOAD PDF KAMILI YA MAJINA HAPA

Leave a Comment